KIFO HAKIKADIRIKI

Nawaza nikiwazuwa, Natetema nikituwa
Napika nikipakuwa, Nachimba nikichimbuwa
Siwezi kuitambuwa, na wala kuichaguwa
Siku ya hatima kuwa, nilale bila kujuwa
Kifo hakikadiriki.

Waje wanaonijuwa, walie bila kutuwa
Waseme hawakujuwa, kifo kimewashutuwa

‘Ni juzi tu akifuwa, pamoja na Bi. Saluwa’
‘Na jana akivuwa, samaki kwenye mashuwa’
Kifo hakikadiriki.

Zianze zangu hatuwa, kuoshwa kwa umuruwa
Na marashi ya viluwa, mwilini pia kifuwa
Wale tende na haluwa, huku wakisoma duwa
Mauti sikuchaguwa, ghafula menichukuwa
Kifo hakikadiriki.

Mali sitoichukuwa, wana sitowasumbuwa
Amali ndo’ kutambuwa, mateso au kutuwa
Si fulani kaniuwa, wala sio kibaruwa
Jalali kashaamuwa, roho yangu kuchukuwa
Kifo hakikadiriki.

Nipelekwe kwa hatuwa, msikitini kwa duwa
Kisha watanichukuwa, kaburini kwa kutuwa
Nisilitambue juwa, au inyeshapo mvuwa
Laiti mungalijuwa, mauti hayana dawa
Kifo hakikadiriki.

 

Malenga – FaFi

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s