Mahaba

Watu usiku hulala, mimi huketi kalia
Aliyonifanya jana, wala sikutarajia
Ghafula amenikana, moyoni kanisusia
Lipi kwake sijafanya, yote nimemalizia
Na sikufanya khiyana, kwake sikumpimia
Mahaba kila aina, tena mia fil mia
Jee huu ni ungwana, yeye kunikatalia?
Mapenzi hayana mana, kwangu yameniishia

– FaFi

One thought on “Mahaba

  1. Pole FaFi kwa kulia, haya hayajanza jana
    Ndio mwendo wa dunia, binadamu kutendana
    Heri penzi kupimia, kwa mja hana amana
    Nafsi yako jilindia, hadhari iwe ndo zana

    Like

Leave a comment